Somalia yaishutumu Ethiopia kwa uvamizi 'haramu'
25 Juni 2024Balozi wa Somalia wa katika Umoja wa Mataifa Abukar Dahir Osman amesema matukio yasio ya kawaida ya hivi karibuni ya Ethiopia yamelisababishia taifa lake kuahirisha hatua ijayo ya uondokaji askari wa ATMIS uliopaswa kuanza Julai hadi Septemba.
Takriban askari 3,000 wa Ethiopia wameweka kambi katika eneo la Pembe ya nchi ya Afrika kama sehemu ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Afrika (ATMIS) unaopambana na Kundi la al Shabaab, wanamgambo ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya Somalia.
Somalia yataka mchakato wa kuondoka vikosi vya ATMIS ucheleweshwe
Uhusiano kati ya serikali za Mogadishu na Addis Ababa ulizorota tangu mwanzo wa mwaka huu baada ya Ethiopia isiyo na bandari kukubali kukodisha kilometa 20 ya ukanda wa pwani kutoka Somaliland sehemu ya Somalia ambayo inataka kujitenga.