Michael Martin ajiondoa.
19 Mei 2009Spika wa Bunge la Uingereza Michael Martin ametangaza leo kuwa atajiuzulu tarahe 21 mwezi ujao kutokana na kulaumiwa kwa kushindwa kufanya mageuzi ambayo yangeliwezesha kuepusha kashfa ya gharama za wabunge.
Hii ni mara ya pili kwa Spika wa Bunge la Uingereza House of Commons kujiuzulu katika historia ya nchi hiyo. Mara ya kwanza ilikuwa miaka 300 iliyopita.
Spika Michael Martin atang'atuka kutokana na lawama kali zilizotolewa baada ya Spika huyo kushindwa kuchukua hatua za kuepusha kashfa ya gharama za wabunge.
Baadhi ya wabgunge wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo walidai kurudishiwa fedha za gharama zao hata kama walinunua mahitaji kama shuka za nyumbani. Wabunge wengine walidai kurududishiwa fedha mara kadhaa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Telegraph pana wabunge waliodai kurudishiwa fedha za gharama za mabwawa ya kuogelea na gharama zilizotokana na matengenezo ya viwanja vya tennis
Akitangaza kujizulu,Spika Michael Martin amesema ameamua kujiuzulu wadhifa wa Uspika Jumapili ya tarehe 21 mwezi juni
Wabunge 23 kutoka vyama vyote hawakuwa na imani na Spika huyo.
Kiongozi wa chama cha upinzani David Cameron ambae kwa sasa anaongoza katika kura maoni amesema wananchi wa Uingereza waliokasirishwa sana wanataka zaidi kupatiwa fursa ya kupiga kura kuliko kuondolowa kwa Spika.Uchaguzi wa bunge nchini Uingereza utafanyika mwezi juni mwaka ujao.
Mwandishi/Mtullya Abdu.
Mhariri/ Mohammed Abdul- Rahman