1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamerhe: "Niko nyuma ya Bujakera"

9 Novemba 2023

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Vital Kamerhe amesema jana kwamba anamuunga mkono mwandishi wa habari ya Kongo Stanis Bujakera anayezuiliwa mjini Kinshasa.

https://p.dw.com/p/4Yahc
Demokratische Republik Kongo Kinshasa | Cherubin Okende
Ripoti juu ya Waziri wa zamani wa usafirishaji Cherubin Okende (katikati) ndio imemtia mashakani mwandishi huyo wa habati Stanis BujakeraPicha: Samy Ntumba Shambuyi/AP/picture alliance

Vital Kamerhe, amesema kiongozi wa taifa pamoja na mamlaka ndio wanaweza kuzungumzia haki za mwandishi huyo anayezuiliwa kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo, katika chapisho lake kwenye gazeti la Jeune Afrique.

Bujakera amekuwa kuzuizini tangu Septemba 8 baada ya kuandika taarifa inayohusiana na kifo cha Cherubin Okende aliyekuwa waziri wa usafirishaji, ambaye mwili wake uliokotwa huko Kinshasa, Julai 13.

Kamerhe amesema ana imani kwamba Bujakera anaweza kuachiliwa huru, ingawa alijizuia kuzungumzia juu ya kesi inayoendelea dhidi ya mwandishi huyo.