1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier India

19 Novemba 2008

Waziri wa nje wa ujerumani amefunga safari ya siku 3 nchini India.

https://p.dw.com/p/FxuZ
Frank-Walter Steinmeier (alipomtembelea Kiongozi/Pakistan)Picha: picture-alliance/dpa

Waziri wa nje wa Ujerumani Bw.Frank-Walter Steinmeier, amefunga safari ya India hii leo kwa ziara ya siku tatu humo nchini.Mada kuu atazozungumzia mjini New Delhi ,ni msukosuko wa fedha ulimwenguni na maswali ya kinuklia.Pamoja na viongozi wa India,Bw.Steinmeier atazungumza pia mchango wa nchi zinazoinukia kiuchumi kama India na China katika kuimarisha na kustawisha uchumi duniani pamoja na jinsi ya kupambana na uchafuzi wa hali ya hewa.

Akifuatana na ujumbe mkuu wa wanabiashara na wa utamaduni, waziri wa nje wa Ujerumani atakuwa na mazungumzo kesho na waziri mkuu wa India ,Manmohan Singh ambae wiki iliopita tu, alikutana na Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani katika mkutano wa kilele wa dola 20 zilizoendelea mno kiviwanda duniani mjini Washington.

Mbali na waziri mkuu huyo, Bw.Steinmeier atazungumza na waziri mwenzake wa mambo ya nje Mukherjee pamoja pia na viongozi wa Upinzani ,Jumuiya za kiraia na hata wa vyama vya wafanyikazi.

Waziri wa nje wa India Mukherjee ,alitia saini mwezi uliopita tu a huko Washington ,Mapatano na Marekani, ambayo yamekomesha marufuku yaliodumu miaka 30 ya kutouziwa India vifaa vya ufundi wa kinuklia . India kwa upande wake, ikaridhia baada ya kusitasita kwa muda mrefu kuruhusu ukaguzi wa kimataifa wa vinu vyake vya kinuklia visivyotumika kijeshi. India, haikuridhia kuingiza vinu vyake vya kijeshi.Na hii imezusha hofu kwamba itapalilia mashindano ya silaha za kinuklia barani Asia.

Msemaji wa maswali ya upunguzaji silaha wa chama cha Upinzani cha kiliberal (FDP) Elke Hoff, amemtaka waziri wa nje Steinmeier kuitaka India kuridhia hatua za kupunguza silaha.

Kabla hakurejea ijumaa hii, Bw.Steinmeier atasfuingua Afisi ya Ubalozi mdogo wa Ujerumani (Konsulat) mjini Bangalore, shina la la teknolojia la India,kusini mwa nchi hiyo.Hiyo itakua afisi ya kwanza ya uwakilishi wa nchi ya nje mjini humo.Lakini tayari kuna afisi za biashara huko.Bangalore ambayo inaitwa Silicon Valley ya India na shina la viwanda vyake vya umeme ,kuna zaidi ya viwanda 120 vya kijerumani au vya ushirikiano baina ya Ujerumani na India.

Kima cha biashara kati ya India na Ujerumani kimeongezeka maradufu mnamo miaka 3 iliopita na kufikia thamani ya dala bilioni 12.Kama kitambulisho cha hamu kuu ya India nchini Ujerumani ni India kuwa mtembezi mkuu katika maonesho mbali mbali -mfano maonesho ya viwanda ya Hannover-Messe,maoneshi ya vitabu ya Frankfurt 2006 na ya Utalii ITB mjini Be