STOCKHOLM.Mwandishi wa Uturuki apokea tuzo ya Nobel ya uandishi fasihi
12 Oktoba 2006Mwandishi kutoka nchini Uturuki Orhan Pamuk ametunukiwa tuzo ya Nobel ya uandishi fasihi ya mwaka huu.
Jopo la mji wa Stockholm nchini Sweden limeusifu moyo wa bwana Pamuk wa kuyachomoza mambo ya nchi yake na ambayo yamewezesha kutoa sura mpya katika tamaduni za kituruki.
Mapema mwaka huu mahakama ya Uturuki ilitupilia mbali kesi iliyomkabili mwandishi huyo baada ya kufikishwa mahakamani kwa kile kilichotajwa kuivunjia hadhi Uturuki kwa kusema katika mahojiano ya televisheni kuwa hakuna mtu nchini mwake ambae anazungumzia waziwazi mauaji ya mamilioni ya wa Armenia ya karne moja iliyopita.
Nchi za umoja wa ulaya zilipiga kelele juu ya mashtaka hayo ambayo yalikiuka uhuru wa mtu kutoa maoni yake nchini Uturuki nchi ambayo inatarajia kujiunga na umoja huo.
Bwana Orhan Pamuk juu ya ushindi wake alisema.
O ton…..Licha ya ulimi wangu mkali ninapenda kuwa mwandishi wa kwanza wa kituruki ambae hatakwenda jela kwa matamshi yake…kwa hilo najivunia sana.
Wakati huo huo Bunge la Ufaransa limepitisha sheria ya kuwa kosa iwapo mtu atakanusha mauaji hayo ya wa Armenia waliouwawa nchini Uturuki. Uamuzi huo umesababisha mivutano kati ya Uturuki na Ufaransa.