STRASBOURG:Huenda serikali ya ujerumani ikawa ya vyama vya CDU/SPD asema Schröder
28 Septemba 2005Matangazo
Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani ameliambia bunge la ulaya mjini Strasbourg kwamba serikali ijayo huenda ikawa ya muungano wa vyama vikuu baina ya chama chake cha Social Demokrats na Christian Demokrats cha wahafidhina.
Hata hivyo Schröder ameonya kwamba huenda ikachukua muda kabla ya kufikiwa makubaliano.
Schröder matokeo ya uchaguzi mkuu wa hivi karibuni yalikuwa ni sawa na kura ya imani juu ya mageuzi ya serikali yake.
Hali inavyoonekana hadi kufikia sasa hakuna kati ya vigogo wawili wa kisiasa Agela Merkel wa CDU na Schröder wa SPD aliyetayari kumuachia mwingine madaraka ya Ukansela kwenye serikali ya mseto inayotarajiwa kuundwa.
Mazungumzo ya pili baina ya vyama hivyo viwili yataendelea hii leo.