Sudan itatumia pato la biashara ya dhahabu kufidia bajeti
24 Januari 2022Matangazo
Hayo yamefanyika wakati Sudan wiki iliyopita ikipitisha bajeti mpya ya mwaka huu 2022 bila ya msaada wa kigeni kufuatia vikwazo baada ya mapinduzi.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya fedha, Serikali imetowa maelekezo mapya yanayoagiza asilimia 70 ya fedha za mapato yanayotokana na biashara ya nje ya dhahabu itumiwe kununua bidhaa muhimu ambazo ni pamoja na mafuta na mtama.
Sudan ambayo ni moja ya nchi za Afrika zinazochimba kwa wingi dhahabu katika kipindi cha miezi 9 ya mwanzo wa mwaka 2021 ilisafirisha tani 26.4 za dhahabu na asilimia 25.2 katika kipindi chote cha mwaka 2020 kwa mujibu wa data za benki kuu ya nchi hiyo.
Hata hivyo maafisa wamekadiria kwamba kiasi kikubwa cha madini hayo kiliuzwa kwa magendo katika nchi za nje.