1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden yawaondoa mabingwa watetezi Marekani

6 Agosti 2023

Sweden imewaduwaza Marekani kwa kuwafunga penalti 5 - 4 na kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake. Hii ni hatua ya mapema kabisa kwa mabingwa hao watetezi kuondolewa katika mashindano hayo.

https://p.dw.com/p/4Upef
Timu ya taifa ya soka la wanawake ya Sweden
Timu ya taifa ya soka la wanawake ya Sweden Picha: Joel Carrett/AAP/IMAGO

Sweden sasa watakutana na Japan Ijumaa. Marekani walitawala kipindi kirefu cha mchezo lakini wakashindwa kuliona lango huku kipa wa Sweden akipangua makombora kadhaa.

Soma zaidi: Kombe la Dunia la Wanawake limevutia wengi

Matarajio yalikuwa juu kwa mabingwa hao mara nne kabla ya kuanza mashindano hayo, ambao walikuwa wametinga angalau nusu fainali katika kila Kombe la Dunia. Katika mikwaju ya penalti ya kuamua mshindi, kila upande ulikosa mikwaju minne. Na mkwaju wa ushindi wa Sweden uliamuliwa kwa mapitio ya video - VAR kuhakikisha kuwa mpira ulikuwa umevuka mstari wa lango.

Mapema leo, wawakilishi wa Afrika, Afrika Kusini walifungasha virago baada ya kufungwa 2 - 0 na Uholanzi ambao wamejikatia tiketi ya kucheza robo fainali dhidi ya Uhispania Ijumaa ijayo.