SiasaSyria
Zaidi ya watu 4,360 wameuawa nchini Syria mwaka 2024
31 Desemba 2023Matangazo
Kulingana na shirika la haki za binaadamu la Syria mapema leo, idadi hiyo imeongezeka, ikilinganishwa na mwaka 2022, ambapo watu 3,825 waliuawa.
Idadi ya mwaka 2022, ilikuwa ni ya chini kabisa tangu mzozo ulipoanza mwaka 2011, baada ya hatua kali za serikali dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakipigania demokrasia.
Idadi ya mwaka huu inajumuisha raia 1,889, wakiwamo wanawake 241 na watoto 307, shirika hilo lenye makao yake nchini Uingereza limesema.
Lakini vikosi vya Syria vimesema ni watu karibu 900 waliokufa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na wapiganaji wa muungano wa kikosi cha jeshi cha SDF kinachoungwa mkono na Marekani, makundi yanayoungwa mkono na Iran, makundi ya Kiislamu, Dola la Kiilslamu na wapiganaji wa kigeni.