1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yatakiwa kujenga upinzani imara

1 Novemba 2012

Marekani imetoa wito wa kufanyiwa mabadiliko uongozi wa upinzani nchini Syria, ikisema kuwa muda umefika sasa kupiga hatua na kuwaingiza wale wanaopigana katika mstari wa mbele wa mapambano nchini humo.

https://p.dw.com/p/16aqe
epa03452479 US Secretary of State Hillary Clinton addresses the media during a joint news conference after meeting with members of Bosnia's tripartite presidency, Muslim Bakir Izetbegovic, Croat Zeljko Komsic and Serb Nebojsa Radmanovic in Sarajevo, Bosnia and Herzegovina 30 October 2012. EPA/FEHIIM DEMIR
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary ClintonPicha: picture-alliance/dpa

Wachunguzi wa masuala nchini Syria pamoja na waasi,wanasema kuwa ongezeko la mashambulizi ya anga yanayofanywa na jeshi la serikali ni jaribio la utawala wa Rais Bashar al-Assad kugeuza mafanikio waliyoyapata waasi.

Ndege za kivita zimeshambulia katika maeneo ya vitongoji vya mji unaoshikiliwa na waasi wa Harasta, mashariki ya mji mkuu Damascus, wakati helikopta za kijeshi zilishambulia wilaya moja ya mji huo mkuu leo.

A general view shows destruction in the Suleiman al-Halabi nieghbourhood, now under full army control according to state media, in the northern Syrian city of Aleppo on October 30, 2012. Explosions shook Syria's capital as warplanes launched their heaviest air raids yet and two car bombs struck, with the UN-Arab League peace envoy saying the conflict was going from bad to worse. AFP PHOTO / STR (Photo credit should read -/AFP/Getty Images)
Mapambano ya silaha mjini DamascusPicha: AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria , jeshi la anga pia limeshambulia miji katika jimbo la kaskazini magharibi la Idlib, ambalo sehemu kubwa ya jimbo hilo inadhibitiwa na waasi.

Ghasia hizo zimekuja siku moja baada ya watu karibu 152 kuuwawa nchini Syria, 58 wakiwa ni raia, 48 ni waasi na wanajeshi wa serikali 46, limesema shirika hilo la haki za binadamu.

Mashambulizi ya anga , wamesema wadadisi wa mambo kuwa hayaelekezwi zaidi dhidi ya waasi lakini yanasababisha hofu kubwa miongoni mwa raia na kuchochea hasira kwa raia wa kawaida ili kupambana na wapiganaji waasi waliomo miongoni mwao.

Mafanikio ya wapiganaji

Wapiganaji wamepata mafanikio kadha katika wiki chache zilizopita, hususan upande wa kaskazini, na jeshi la anga la Syria linaona hali hii kuwa ni kitisho, amesema Charles Lister, mchambuzi mwenye makao yake makuu mjini London anayefanyakazi na kituo cha IHS Jane, kinachohusika na masuala ya uchunguzi wa ugaidi na mapambano ya wapiganaji.

Clinton aonya

Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton , akitoa ishara ya kuchukuliwa hatua imara zaidi na serikali ya Marekani katika juhudi za kuunda upinzani wa kisiasa wenye kuaminika dhidi ya rais wa Syria Bashar al-Assad, amesema kuwa mkutano utakaofanyika wiki ijayo nchini Qatar utakuwa nafasi ya kupanua muungano wa wapinzani dhidi ya Assad.

"Huu hauwezi kuwa upinzani unaowakilishwa na watu ambao wana malengo mengi tu mazuri , lakini kwa wakati mwingi hawajakuwa ndani ya Syria kwa zaidi ya miaka 20,30, au 40," amesema Clinton wakati wa ziara yake nchini Croatia.

Clinton pia ameonya kuwa Marekani inahitaji kuusaidia upinzani nchini Syria kuungana na kupambana na utawala wa rais Bashar al-Assad, lakini ameutaka upinzani kujitenga na juhudi za wale wenye msimamo mkali ambao wanataka kuteka mapinduzi ya nchi hiyo.

A Syrian army fighter jet flies over the northern city of Aleppo on October 13, 2012. Syrian rebels shot down a fighter jet in Aleppo a monitoring group and a military defector said, as fierce fighting in the region continues. AFP PHOTO/TAUSEEF MUSTAFA (Photo credit should read TAUSEEF MUSTAFA/AFP/GettyImages)
Jeshi la anga la Syria likifanya mashambulio mjini AleppoPicha: AFP/GettyImages/Tauseef Mustafa

Matamshi ya Clinton yanawakilisha mtazamo wa kuachana na baraza la taifa la Syria, SNC, ambalo ni kundi lililopo nje ya nchi, kundi ambalo limekuwa likitoa matamshi ya kupinga kuingilia kati kwa jumuiya ya kimataifa katika mzozo nchini Syria.

Maafisa wa Marekani wamekuwa wakieleza pembeni kutoridhishwa kwao na uwezo wa baraza hilo la taifa la Syria , kuja pamoja na mpango wenye kueleweka na kushindwa kwao kuyaunganisha makundi ya ndani ya Syria ambayo yamekuwa yakipambana kwa muda wa miezi 19 sasa dhidi ya utawala wa Assad.

Wanachama waandamizi wa baraza la taifa la Syria, jeshi la ukombozi wa Syria FSA na makundi mengine ya waasi yamemaliza mkutano wao nchini Uturuki jana na kupendekeza muungano wa serikali ya mpito katika miezi ijayo.

"Ni mgawanyiko uliopo kwetu ambao umeruhusu majeshi ya Assad kufikia hadi hapa tulipo", Amesema Ammar al-Wawi , kamanda wa jeshi la waasi , ameliambia shirika la habari la reutres baada ya mazungumzo nje kidogo ya mji mkuu Istanbul.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe

Mhariri: Mohammed Khelef