1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Türk aikosoa vikali kauli ya Waziri wa fedha wa Israel

9 Agosti 2024

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amemkosoa vikali Waziri wa fedha wa Israel Bezalel Smotrich.

https://p.dw.com/p/4jIdt
Volker Türk | Hohe Kommissar der Vereinten Nationen für Menschenrechte
Picha: Kyodo News/IMAGO

Türk amemkosoa Smotrich kuhusu kauli yake yenye utata kwamba ni haki kusababisha njaa kwa Wapalestina.

Mkuu huyo amesema kauli kama hizo zinachochea chuki dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.

Ameeleza kwamba, kuwasababishia watu njaa ni uhalifu wa kivita na kwamba kauli kama hizo zinazotolewa na viongozi waandamizi zinafaa kukoma na kuchunguzwa, na iwapo mtu atapatikana na hatia anapaswa kufunguliwa mashtaka na kuadhibiwa.

Kulingana na vyombo vya habari vya Israel, Smotric alisema ni haki kuzuia misaada ya kibinadamu kwenda Gaza hadi mateka ambao bado wanashikiliwa na kundi la Hamas watakapoachiliwa hata kama hatua hiyo itamaanisha Wapalestina milioni mbili wangekufaa kwa njaa.