1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taarifa ya UNESCO

Omar Babu26 Oktoba 2006

Ripoti ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, imesema ukuaji wa mamilioni ya watoto katika mataifa yanayoendelea unatatizika kutokana na ukosefu wa uangilizi bora unaozingatia afya bora na lishe.

https://p.dw.com/p/CHmF
Nembo ya Umoja wa Mataifa
Nembo ya Umoja wa Mataifa

Shirika la elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa mataifa, UNESCO, linasema mipango ya afya na lishe bora inachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza viwango vya vifo miongoni mwa watoto.

Shirika hilo aidha linasisitiza kuwa mipango hiyo hutoa njia mwafaka ya kuwaanda watoto hao kwa maisha yao ya usoni.

Mwaka 2004 asilimia 37 ya watoto walihudhuria shule za chekechea zinazowahudumia watoto wa kati ya miaka mitatu na miaka sita.

Idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na asilimia 17 mwaka elfu moja mia tisa na sabini na tano ingawa haijaafikia kiwango ambacho Umoja wa Mataifa unatarajia.

Kwa mujibu wa UNESCO, mipango ya utunzaji wa watoto wachanga wenye umri chini ya miaka mitatu haipatikani katika zaidi ya nusu ya mataifa ambayo watoto hubaki kwenye himaya ya wazazi wao au jamii zao.

Taarifa hiyo imetahadharisha kuwa katika mataifa yanayoendelea mshikamano uliokuwepo wa kijamii umedhoofishwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaofanya kazi, uhamaji kutoka vijijini kuelekea mijini pamoja na janga la Ukimwi.

Kwenye taarifa hiyo Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Koichiro Matsuura ametoa wito wa kutumiwa uwezo wa kisiasa kuimarisha mipango ya afya bora na pia elimu kwa watoto wachanga.

Taarifa hiyo inawataja watoto kuwa kiungo muhimu kilichotelekezwa katika mfumo mzima wa elimu.

Matsuura amesema suala la malezi mema kwa watoto katika umri wao mdogo ni lazima lijumuishwe sera za elimu na pia sera za kukabiliana na umaskini.

Suala la kupanua na kuimarisha mipango ya afya bora na elimu kwa watoto lilikuwa miongoni mwa malengo sita yaliyowekwa katika kongamano la Umoja wa Mataifa mwaka 2000 mjini Dakar

Watoto kiasi cha milioni kumi na laki tano walio na umri chini ya miaka mitano hufa kila mwaka duniani kutokana na maradhi yanayoweza kukingwa. Maeneo ya Afrika kusini ya Jangwa la Sahara pamoja na Eshia ya Magharibi ndiyo yaliyothirika zaidi.

Kulingana na taarifa hiyo ya UNESCO, Amerika Kusini inaongoza orodha miongoni mwa mataifa yanayoendelea kwa kuwa na asilimia 62 ya watoto kwenye shule za chekechea.

Eneo hilo pia limefanikiwa kupunguza utapiamlo miongoni mwa watoto kutokana na miradi yake ya kushughulikia watoto wa umri mdogo.

Eneo la Afrika, kusini ya jangwa la Sahara lina asilimia 12 ya watoto waliosajiliwa kwenye shule za chekechea ikilinganishwa na asilimia 16 katika mataifa ya kiarabu, asilimia 32 katika Eshia Kusini na Magharibi na asilimia 35 katika eneo la Eshia Mashariki na Pacific.

Barani Ulaya na Amerika Kaskazini suala la kuwapeleka watoto kwenye shule za chekechea limezingatiwa kwa kiasi kikúbwa kutokana na idadi inayoongezeka ya wanawake wanaofanya kazi na pia watoto walio na mzazi mmoja.

Huku likizingatia maeneo maskini zaidi duniani Shirika la UNESCO, limeyataka mataifa husika kuongeza fedha zaidi kwenye miradi ya malezi ya watoto wachanga.

Kwa sasa hivi fedha zinazogharamia chekechea ni chini ya asilimia kumi ya fedha zilizotengewa sekta