Pato la taifa Ujerumani kunywea hadi asilimia 0.5 mwaka 2023
29 Agosti 2023Hali hiyo imetokana na viwango vya juu vya riba, bei za nishati zilizoongezeka na mauzo duni ya bidhaa za nje.
Katika ripoti yake mpya, taasisi hiyo imesema uchumi wa Ujerumani umeathirika hasa kutokana na siasa za kikanda kama vile mzozo wa Ukraine na mivutano yake na China.
Taasisi hiyo ya uchumi inatabiri kuwa, pato jumla la Ujerumani mwishoni mwa mwaka huu 2023 litakuwa sawa kama ilivyokuwa mwaka 2019. Kwa wastani, taasisi hiyo ya IW inataraji kuwepo na watu milioni 2.58 wasiokuwa na ajira mwaka huu 2023, idadi hiyo ikiwa watu 160,000 zaidi ya mwaka uliopita.
Hali hiyo itasababisha kiwango cha ukosefu wa ajira kuongezeka hadi asilimia 5.5.
Kwa ujumla, kiwango cha mfumuko wa bei mwaka 2023 kitakuwa chini kidogo ya kiwango cha mwaka uliopita kwa asilimia 6.5.