1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUbelgiji

Tadesco amwaga wino Ubelgiji

8 Februari 2023

Shirikisho la Soka la Ubelgiji limemteua Domenico Tedesco kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji kuchukua nafasi ya Roberto Martinez.

https://p.dw.com/p/4NFCU
RB Leipzig - 1. FC Union Berlin
Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Tadesco raia wa Italia mwenye umri wa miaka 37 ametia saini mkataba hadi baada ya michuano ya Kombe la Euro 2024 itakayoandaliwa nchini ujerumani. Kocho huyu amewahi kuzinoa Schalke 04, Spartak Moscow na Leipzig.

SOMA PIA: Domenico Tedesco amwaga wino RB Leipzig

Martinez, ambaye aliongoza Ubelgijikumaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Dunia mnamo 2018.

Amekuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Ubelgiji kwa miaka sita na alijiuzu baada ya Red Devils kushindwa kutinga hatua ya mtoano katika mashindano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Kuondoka kwa Martinez kuliambatana na uwezekano wa kuvunjika kwa kinachojulikana kama ``Kizazi cha Dhahabu,'' cha Ubelgiji enzi iliyohusisha washambuliaji wakubwa wachezaji kama Kevin De Bruyne, Eden Hazard, Romelu Lukaku na Dries Mertens.

Jukumu kubwa la Tesdesco litakuwa kujenga upya kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji kabla ya michuano ya Kombe Ulaya.

Kampeni ya Ubelgiji ya kufuzu kwa Euro 2024 inaanzia na mechi dhidi ya Uswidi mnamo Machi 24.