Taifa Stars kupimana nguvu na Morocco AFCON
17 Januari 2024Mioyo ya mashabiki wengi wa soka inadunda dunda wanapotambua kwamba Taifa Stars iko machoni mwa wakali wa soka barani Afrika, lakini hilo wanaliweka kando na wanasema kama ilivyo kwa fyekeo linaweza kung'oa lundo la nyasi kwa wakati mmoja , basi hilo linawezekana pia kwa Morocco kuondoka dimbani huku wakiwa vichwa wameimanisha chini.
Kila kona upitapo hamasa kuhusu mchezo wa leo iko juu na mazungumzo mengi ni kuhusu Taifa Stars inavyoweza kuishangaza Afrika, kama ilivyoshuhudiwa kwa timu nyingine zilivyoweza kuwatoa jasho magwiji wa soka barani humu.
Baadhi ya mashabiki waamamini kwamba iwapo wachezaji wa Stars watakaza mikwiji yao bara bara na kuweka kando hufu ya kukutana na wachezaji vigogo basi wataweza kutoa zaiwadi yao ya kwanza kwa Watanzania tangu timu hiyo ianze kushiriki michuano hiyo ya Afrika.
Kimehesabu Taifa Stars inakumbana na timu yenye rekodi ya hali yua juu katika viwango vya ubora wa Fifa na kwamba itakuwa inaingia dimbani ikilijua jambo hilo.
Baadae Taifa stars watachuana na Zambia
Lakini baadhi ya mashabiki wanapata matumaini na matokeo ya mchezo wa jana wakati Namibia inayoshika rekodi ya nafasi ya 112 katika viwnago vya ubora duniani, ilipoiangusha Tunisia kwa bao 1-0 ambayo kwa mujibu wa viwnago vya Fifa iko nafasi ya 28.
Hata hivyo, hayo tisa, kumi Taifa Stars inavaana na timu iliyovunja rekodi ya Afrika kwa kuwa timu ya kwanza kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Qatar. Mashabiki wanasema mfalme uliyevuma jana hawezi kuendelea kuvuma wakati wote.
Kwa sasa kila mmoja macho anayoelekea huko Ivory Coast akisubiri muda wa saa mbili usiku kushuhudia mtangane huo unaongejewa kwa hamu kubwa. Lakini baadhi wanaonyesha wasiwasi huenda wasifaidi kuufulia mchezo huo moja kwa moja kutokana na kadhia inayoshuhudiwa sasa ya kukatika umeme mara kwa mara.
Baada ya mchezo wake wa leo, Taifa Star itabidi isubiri hadi mwishoni mwa wiki kuvaana na Zambia ambayo nayo leo inavaana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika michezo ya kundi F.
Mwandishi: George Njogopa