Taiwan na Marekani kuanza upya mazungumzo ya biashara
30 Juni 2021Mazungumzo hayo yamerejea baada ya pande mbili kuitisha tena Baraza la Makubaliano ya Mfumo wa Biashara na Uwekezaji - TIFA, ambalo wakati wa utawala wa rais wa zamani Barack Obama, lilikuwa na dhamana ya kutafuta njia za kuimarisha uhusiano.
Baraza hilo lilikutana kwa mara ya mwisho mwaka 2016 kabla ya kuchaguliwa kwa Donald Trump, ambaye alibadilisha mwelekeo na kujikita kwenye kufikia makubaliano makubwa na China, ingawa uhusiano kati ya Washington na Beijing ulidorora pakubwa kufikia mwishoni mwa muhula wake uliogubikwa na machafuko.
Mazungumzo yamejikita juu ya kupeleka mbele uhusiano na muda mrefu wa biashara na uwekezaji kati ya Marekani na Taiwan, imesema taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani.
Mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao na kuongozwa kwa pamoja na maafisa wa juu wa biashara kutoka Washington na Taipei.