Tanzania, katiba mpya na Muungano
11 Juni 2013Matangazo
Katika kipindi hiki cha Maoni mbele ya Meza ya Duara, Mohammed Abdulrahman wa Idhaa ya Kiswahili ya DW anaongoza mjadala unaowashirikisha Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valerie Msoka, mwanasiasa mkongwe na mmoja wa waasisi wa hoja ya Muungano wa Serikali Tatu, Njelu Kasaka, mwakilishi wa Mji Mkongwe na mmoja wa watetezi wa Mamlaka Kamili ya Zanzibar, Ismail Jussa, na mbunge wa CHADEMA, John Shibuda.
Kusikiliza mjadala huu, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mhariri: Mohammed Khelef