1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tawheed Jamaat wanyoshewa kidole cha lawama Sri Lanka

Oumilkheir Hamidou
23 Aprili 2019

Wasrilanka milioni 21 wamekaa kimya dakika tatu kuomboleza na kuwakumbuka zaidi ya watu 300 waliouwawa katika mashambulio ya mabomu ya jumapili ya pasaka, Zaidi ya 500 wengine wamejeruhiwa

https://p.dw.com/p/3HGVI
Relatives of victims react at a police mortuary following bomb blasts in Colombo
Picha: Reuters/D. Liyanawatte

Bendera zimeteremshwa nusu mlingoti katika majengo ya serikali na watu kuinamisha vichwa  chini  na kuomboleza kimya kimya kutokana na matumizi ya nguvu yaliyozusha laana za walimwengu. Muda mfupi baada ya dakika tatu hizo za maombolezi hayo, msemaji wa polisi amesema idadi ya waliuwawa imefikia watu 310.

Ibada za kwanza za maiti, wakiwemo dazeni kadhaa ya wageni, zimefanyika pia hii leo,masaa kadhaa baada ya serikali kutangaza sheria ya hali ya hatari na kusema kundi la itikadi kali ya dini ya kiislam ndilo linalohusika na mashambulio hayo.

Naibu waziri wa ulinzi wa Sri Lanka amesema kwa upande wake dalili za mwanzo zinazotokana na uchunguzi zinaonyesha mashambulio hayo yamefanywa ili kulipiza kisasi kwa mauwaji yaliyotokea katika misikiti miwili ya mji wa Christchurch , kusini mwa New-Zealand marchi 15 iliyopita  ambapo watu 50 waliuwawa.

Wanajeshi wasri Lanka wakiwasaka magaidi
Wanajeshi wasri Lanka wakiwasaka magaidiPicha: picture-alliance/dpa/epa/str

Kundi la itikadi kali la Tawheed Jamaat linatuhumiwa kuhusika na mashamabulio hayo

Polisi wanasema watu 40 wanashikiliwa kuhusiana na mashambulio hayo, ya kikatili kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipomalizika nchini Sri Lanka mwongo mmoja uliopita.

Mashambulio hayo ni mabaya kabisa kuwahi kutokea dhidi ya jamii ya wachache ya wakristo wanaofikia asili mia 7 tu ya wakaazi milioni 21 wa Sri Lanka.

Wachunguzi wanataka kujua kama kundi la itikadi kali linalojiita linalotuhumiwa kuhusika na mashambulio hayo- Twauheed Jamaath-NTJ,"limepata msaada kutoka nje" amesema hayo msemaji waserikali Rajitha Senaratne.

Ofisi ya rais Maithripala Sirisena imesema wamepokea habari kwamba makundi ya kigaidi ya kimataifa yamewasidia wahalifu wa ndani na kwamba Srilanka itaomba msaada wa kimataifa kulichunguza suala hilo.

Rais Maithripala Sirisena
Rais Maithripala SirisenaPicha: Getty Images/L. Wanniarachchi

Bunge la Sri Lankia linakutana kuzungumzia masuala yanayojitokeza kama mashambulio hayo yangeweza kuepukwa,.

Maafisa wanachunguza kwanini hatua za tahadhari hazikuchukuliwa baada ya onyo la April 11 kwamba kundi la itikadi kali la Tawheed Jamaat-NTJ wanapanga kufanya mashambulio makanisani.

 Maelezo yanaanza kutolewa kuhusu wageni waliouwawa katika mashambulio hayo: Marekani inasaema raia wake wanne wameuwawa huku Uholanzi ikisema  raia wake watatu wameuwawa. Tajiri mmoja wa Danemark amefiwa na wanawe watatu. Waengereza wanane, wahindi wanane na raia wengine kuitoka Uturuki, Ufaransa, Japan na Ureno  ni miongoni mwa waliouwawa pia.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP

Mhariri: Sekione Kitojo