Asilimia 70 ya wakazi wanaoishi mashambani nchini Kenya wanategemea kilimo. Katika maeneo ambayo yanakabiliwa na ukame na uhaba wa mvua serikali pamoja na mashirika ya kimataifa wanajitahidi kuwahimiza wakulima kupanda mbegu zenye kuhimili ukame kama vile mbaazi, mtama, mawele na kunde. Sikiliza Makala Yetu Leo iliyoandaliwa na Shisia Wasilwa.