SiasaAfghanistan
Tetemeko la ukubwa wa 6.3 lapiga Magharibi mwa Afganistan
7 Oktoba 2023Matangazo
Hadi sasa hakuna taarifa za vifo wala uharibifu wa majengo, lakini taarifa ya Shirika la Utafiti wa jiolojia Marekani imeonya kwamba huenda kukawa na maafa. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika kiwango hicho cha tahadhari kunahitajika mwitikio wa ngazi ya kikanda au kitaifa.
Soma pia:Waliofariki tetemeko la ardhi nchini Morocco yafika 2,901
Itakumbukwa kuwa, mwezi Juni mwaka uliopitazaidi ya watu 1,000 walikufana maelfu waliachwa bila makaazi baada ya tetemeko la ukubwa wa 5.9 ambalo ni baya zaidi nchini humo kwa kipindi cha robo karne kupiga jimbo masikini la Paktika.