Timu ya kampeni ya Kamala Harris yakusanya dola milioni 540
26 Agosti 2024Kiongozi wa timu hiyo ya kampeni Jen O'Malley Dillon amesema kuwa, kabla ya Kamala Harris kutoa hotuba ya kukubali rasmi uteuzi wa chama cha Democratic kuwa mgombea urais siku ya Alhamisi, tayari walikuwa wamekusanya zaidi ya dola milioni 500.
O'Malley ameeleza kuwa, karibu theluthi moja ya michango wiki iliyopita ilitoka kwa wachangiaji waliotoa kwa mara ya kwanza.
Soma pia: Kamala kutoa hotuba ya aina yake kukubali uteuzi
Takriban asilimia 20 ya wachangiaji hao wa mara ya kwanza walikuwa wapiga kura vijana huku theluthi mbili wakiwa wanawake; makundi ambayo yanachukuliwa kuwa muhimu kwa Harris kupata ushindi katika uchaguzi wa mwezi Novemba.
Kampeni hiyo imeshuhudia ongezeko la michango wakati wa kongamano la kitaifa la chama cha Democratic lililofanyika mjini Chicago ambapo Kamala Harris na mgombea mwenza wake, gavana wa Minnesota Tim Walz walikubali rasmi uteuzi wao.