SiasaMarekani
Trump amshambulia kwa maneno mwendesha mashtaka
5 Aprili 2023Matangazo
Trump amejitangaza kuwa mwathiriwa wa kuingiliwa uchaguzi bila kutolewa ushahidi wowote.
Akiwahutubia wafuasi waliokusanyika nyumbani kwake Mar-a-Lago katika mji wa Palm Beach, Florida, Trump amesema hakuwahi kudhani kitu kama kilichoshuhudiwa jana kingefanyika Marekani.
Awali, Trump mwenye umri wa miaka 76 alikanusha mashitaka yote 34 katika Mahakama ya Manhattan ya kughushi nyaraka za kibiashara, wakati waendesha mashitaka wakimtuhumu kwa kupanga malipo kwa wanawake wawili kabla ya uchaguzi wa 2016 ili kuzuia uchapishwaji wa taarifa za kuwa na mahusiano ya kingono naye.