SiasaAsia
Tume ya haki yaonesha wasiwasi wa uchaguzi huru Pakistan
2 Januari 2024Matangazo
Kadhalika tume hiyo imeonesha wasiwasi kuhusu mamlaka kuwazuia wagombea wa chama cha Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan.Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Islamabad, mwenyekiti mwenza wa Tume ya Haki ya Binaadamu ya Pakistani, Munizae Jahangir, amesema pia vyama vingine vya kisiasa vimewekewa mbinu sawa hizo lakini kwa viwango tofauti. Khankwa sasa yuko gerezani anatumikia kifungo cha miaka mitatu baada ya kufikwa na hatia ya rushwa. Pia anakabiliwa na rundo la mashtaka mengine, hali inayoleta ugumu kwake ugombea nafasi ya hiyo.