SiasaPoland
Tusk atetea mpango wa kusitisha haki ya kuomba hifadhi
15 Oktoba 2024Matangazo
Katika ujumbe alioandika katika mtandao wa kijamii wa X, Tusk amesema ni haki na jukumu lao kulinda mpaka wa Poland pamoja na ule waUlaya na kuongeza kuwa usalama wake hautajadiliwa.
Tusk alitangaza mpango huo wake wa kusitisha haki ya wahamiaji kuomba hifadhi wakati wa kongamano la Muungano wake wa Kiraia siku ya Jumamosi. Hiyo ni sehemu ya mpango utakaowasilishwa kwenye kikao cha baraza la mawaziri hii leo Jumanne.
Soma pia;Poland yapanga kusitisha kwa muda haki ya kuomba hifadhi
Hata hivyo uamuzi huo hautawaathiri raia wa Ukraine ambao wamepewa ulinzi wa kimataifa nchini Poland.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takriban watu milioni 1 kutoka Ukraine wamekimbia vita nchini humo kuingia Poland.