Uchaguzi kufanyika katika muda wa miezi miwili au mitatu Anzuan.
1 Aprili 2008Mutsamudu. Comoro.
Uchaguzi wa rais katika kisiwa kilichokombolewa hivi karibuni cha Azouan utafanyika katika miezi miwili ama mitatu kwa mujibu wa rais wa mahakama ya rufaa kisiwani humo Lailizamane Abdou Sheikh ambaye aliapishwa jana kuwa rais wa mpito wa kisiwa hicho.
Abdou Sheikh amewashukuru wanajeshi wa Comoro wakiongozwa na majeshi ya umoja wa Afrika kwa kurejesha amani baada ya kumuondosha madarakani kiongozi muasi kanali Mohamed Bakar.
Shirikisho la muungano wa visiwa vya Comoro lina visiwa vitatu , ikiwa kila kimoja kinatawaliwa na kiongozi wao na bunge, lakini vinaunganishwa katika shirikisho kwa kuwa na rais mmoja.Majeshi ya serikali na yale ya umoja wa Afrika yalivamia kisiwa cha Anzouan na kumuondosha madarakani Mohamed Bakar March 25 baada ya kukataa miito ya kujiuzulu. Alikimbilia kisiwani Mayotte, ikiwa ni kisiwa cha nne , ambacho bado kimo katika udhibiti wa Ufaransa.
Kwa hivi sasa kura hati ya kukamatwa ya serikali dhidi ya bakar ambaye anatakiwa arejeshwe visiwani Comoro kutoka katika kisiwa cha Ufaransa cha Reunion, ambako alipelekwa na kuwekwa chini ya ulinzi kwa madai ya kuwa na silaha kinyume na sheria.