1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi mkuu Kenya ama Disemba 2012 au Machi 2013

Amina Abubakar13 Januari 2012

Mahakama Kuu ya Kenya imetangaza kwamba uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika mwezi Machi 2013 au unaweza ukafanyika mwezi Disemba 2012 ikiwa tu Serikali ya Umoja wa Kitaifa itavunjwa kabla ya wakati huo.

https://p.dw.com/p/13j0q
Rais Mwai Kibaki wa Kenya
Rais Mwai Kibaki wa KenyaPicha: AP

Uamuzi huo wa Mahakama uliotangazwa hivi punde, sasa umetatua mvutano uliokuwepo miongoni mwa wanasiasa juu ya tarehe kamili ya kufanyika uchaguzi.

Uchaguzi huo utakuwa ni wa kwanza kufanyika nchini Kenya tangu ghasia zilizosababisha vifo na uharibifu mkubwa wa mali nchini humo miaka minne iliyopita. Amina Abubakar amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya, Harun Ndubi, kujua je kwanza uamuzi huu una maana gani kwa wananchi wa Kenya.

Mahojiano: Amina Abubakar/Harun Ndubi
Mhariri: Othman Miraji