1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Uchaguzi Mkuu kufanyika Nigeria licha ya uhaba wa fedha

24 Februari 2023

Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria imesema imepokea fedha za kutosha kuendesha uchaguzi utakalofanyika Jumapili na kutupilia mbali wasiwasi kwamba kura hiyo itaahirishwa kwa sababu ya mzozo wa noti nchini humo.

https://p.dw.com/p/4NvW8
Nigeria vor Präsidentschaftswahl | Wählerkarte
Picha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Uhaba huo wa fedha ulizidisha wasiwasi mkubwa kwamba huenda wapiga kura wakapata shida kufika katika vituo vyao vya kupiga kura siku ya Jumamosi. Katika siku za nyuma mamlaka zilichelewesha uchaguzi wa urais, lakini tume huru ya uchaguzi imesema hapo jana kwamba vifaa vya uchaguzi pamoja na rasilimali watu wamepelekwa kwenye vituo vya kupiga kura vipatavyo 175,000 kote nchini Nigeria.

kesho Jumamosi Nigeria taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika linapiga kura kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, baada ya kuhudumu kipindi cha mihula miwili.

Wagombea 18 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo huku wagombea watatu wa usoni wanadi juu ya maisha bora kwa Wanaigeria pamoja na kuimarisha hali ya usalama.