1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yafanya uchaguzi wa urais

15 Machi 2024

Raia nchini Urusi wanapiga kura kuanzia hii leo katika uchaguzi wa urais utakaofanyika kwa siku tatu na unaotarajiwa kumuongezea muda zaidi Rais Vladimir Putin.

https://p.dw.com/p/4dXOd
Urusi | Uchaguzi wa Rais
Moja ya vituo vya kupigia kura Namba 1173 katika kijiji cha Perevalnoye nchini UrusiPicha: Viktor Korotaev/Kommersant/Sipa USA/picture alliance

Uchaguzi huo hata hivyo unafanyika huku kukiwa na ukandamizaji mkubwa dhidi ya upinzani, vyombo huru vya habari na makundi maarufu vya haki za binaadamu na kumfungulia mlango Putin wa kuudhibiti kikamilifu mfumo wa kisiasa.

Raia wanapiga kura kwenye vituo karibu 100,000 kuanzia hii leo Ijumaa hadi Jumapili ndani ya taifa hilo na kwenye maeneo yaliyonyakuliwa na Urusi huko nchini Ukraine katikati ya vita vilivyoingia mwaka wa tatu sasa.

Waangalizi hata hivyo hawatarajii kwamba uchaguzi utakuwa huru na haki kwa kuwa wapiga kura hawana uwanja mpana wa kuchagua.