Uchaguzi wa baraza la seneti wafanyika leo Burundi
28 Julai 2010Matangazo
Uchaguzi wa seneti unafanyika leo nchini Burundi, licha ya vyama vya upinzani vikiususia huku vikilalamika juu ya udanganyifu kutoka kwa serikali. Hapo jana tume ya uchaguzi nchini humo ilitangaza kwamba chama tawala cha rais wa sasa Pierre Nkurunziza, CNDD-FDD kilishinda kwa wingi wa kura uchaguzi uliokamilika wa ubunge. Chama hicho kilijinyakulia viti 81 kati ya 106 bungeni.
Mwandishi wetu Hamida Issa ameandaa taarifa ifuatayo.
Mwandishi, Peter Moss
Mhariri, Josephat Charo