Utafiti uliofanywa na wataalamu wa Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) waliozuru nchini Tanzania unaonesha kuna viashiria vya uchumi wa nchi hiyo kushuka licha ya maafisa wa serikali kusema uchumi umekuwa kwa kiwango cha aslimia 6.8 katika nusu ya mwaka 2017. Isaac Gamba amezungumza na mtaalamu wa masuala wa uchumi nchini Tanzania Professor Honest Ngowi kuhusiana na hilo.