1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchunguzi wa ajali ya treni utafanyika kwa uwazi Ugiriki

9 Machi 2023

Waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis, ameahidi uwazi katika uchunguzi wa ajali mbaya zaidi ya reli iliyosababisha vifo vya watu 57, siku moja baada ya maandamano makubwa kuitikisa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4OSxn
UK Besuch des griechischen Premierminister Kyriakos Mitsotakis in London
Picha: Justin Ng/Avalon/Photoshot/picture alliance

Akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza wa baraza la mawaziri tangu kutokea kwa ajali hiyo, Mitsotakis ameahidi hatua za haraka kuboresha hali ya matatizo katika reli na kwamba atafanya kila linalowezekana kukamilisha uboreshaji wa mifumo ya usalama.
      
Miito ilikuwa inaongezeka kwa Mitsotakis kujiuzulu kutokana na ajali hiyo. 

Wafanyakazi kote Ugiriki wagoma kufuatia ajali ya treni

Mkuu mmoja wa kituo cha treni tayari ameshtakiwa huku duru ya mahakama ikiliarifu shirika la habari la AFP kwamba wasimamizi wengine wawili wa reli pia wameshtakiwa leo kwa mauaji ya uzembe, kusababisha madhara ya mwili na kutatizwa kwa usafiri.