Ufaransa yawahamisha raia wake na wa kigeni
27 Machi 2024Wizara ya Mambo ya Nje a Ufaransa imethibitisha kuhamishwa kwa watu hao, ambao imesema walikuwa kwenye mazingira magumu.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu hao walipelekwa hadi kwenye boti la jeshi la wanamaji ambalo litawasafirisha leo kuelekea Fort-de-France, mji mkuu wa kisiwa cha Carribean cha Martinique, kinachomilikiwa na Ufaransa.
Kulingana na taarifa hiyo, takriban raia 1,100 wa Ufaransa wanaishi Haiti, wengi wao wakiwa na uraia pacha.
Ufaransa ilitangaza kuanza kwa safari hizo za ndege siku ya Jumapili na kusema watu wanaotaka kuondoka nchini Haiti wanapaswa kuwasiliana na ubalozi wake mjini Port-au-Prince.
Port-au-Prince imekumbwa na ghasia za magenge ya uhalifu zilizozuka mwishoni mwa mwezi Februari, na kusababisha kujiuzulu kwa waziri mkuu Ariel Henry mapema mwezi huu.