1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirikisho la Kandanda la Argentina lashutumiwa kwa ubaguzi

17 Julai 2024

Shirikisho la Kandanda la Ufaransa FFF limesema linapanga kuwasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Kandanda Duniani FIFA dhidi ya Argentina kufuatia matamshi ya kibaguzi.

https://p.dw.com/p/4iPUi
Fußball WM Katar Finale | Argentinien v Frankreich
Picha: Yukihito Taguchi/USA TODAY/IMAGO

FFF imesema litawasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Kandanda Duniani FIFA na kufungua kesi dhidi ya Argentina baada ya wachezaji wa timu hiyo kusikika wakiimba wimbo wa kibaguzi baada ya kushinda taji la Copa America. 

Rais wa shirikisho hilo la Ufaransa Philippe Diallo amelaani vikali tukio hilo aliloliita lisilokubalika na matamshi yaliyokuwa yameelekezewa wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Kampeni dhidi ya ubaguzi michezoni

Wimbo na matamshi hayo yalisikika wakati mchezaji wa Argentina na klabu ya Chelsea Enzo Fernandez alipochapisha ukanda wa video katika mtandao wa kijamii wakati wachezaji wa timu hiyo ya taifa walipokuwa kwenye basi lao wakisherehekea ushindi wao dhidi ya Colombia.

Baadhi ya wachezaji akiwemo Fernandez walikuwa wanaimba wimbo dhidi ya Ufaransa wakimlenga Kylian Mbappe.

Wimbo huo uliolaaniwa wakati huo, waliuimba baada ya kuwashinda Ufaransa katika fainali ya Kombe la dunia mwaka 2022.