SiasaMarekani
Marekani yakaribisha mazungumzo kati ya Xi na Zelenskiy
26 Aprili 2023Matangazo
Hata hivyo Washington imetadharisha kuwa bado ni mapema kufahamu iwapo yatasaidia kuleta amani.
Ufaransa ilikuwa nchi ya kwanza kusifu mazungumzo hayo ikisema inaunga mkono juhudi zote zitakazosaidia kumaliza vita vya Ukraine na ambazo zinazingatia maslahi ya serikali mjini Kyiv na sheria ya kimataifa.
Kwa upande wake msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa nchini Marekani John Kirby amewaambia waandishi habari kuwa mazungumzo kazi ya Xi na Zelensky ni jambo zuri lakini haijabainika kama yatakuwa na mchango wa kumaliza vita.
Mazungumzo hayo ya viongozi hao wawili yameshuhudia Ukraine ikimteua balozi mpya wa China na rais Xi Jinping akiahidi kumtuma mjumbe wa amani kuitembelea Kyiv kufungua njia ya mashaurino ya kuushughulikia mzozo unaoendelea