Ufaransa, Ujerumani, Uingereza zalaani Iran kuhusu nyuklia
15 Juni 2024Washirika hao watatu wamesema hatua za Irak zinadhoofisha makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kuhusu mpango wake wa nyuklia. IAEA ilisema siku ya Alhamisi kwamba Iran ilikuwa inaimarisha urutubishaji wa madini ya urani katika vituo vyake viwili.
Ukosoaji huo unajiri zaidi ya wiki mbili baada ya mataifa hayo kuwasilisha azimio katika mkutano wa bodi ya magavana wa IAEA, linalokosoa kukosekana kwa ushirikiano na shirika hilo kutoka kwa Iran, katika hatua ya kwanza kama hiyo tangu Novemba 2022.
Soma pia: Iran yasema mazungumzo na mkuu wa IAEA yalikuwa mazuri
Iran ililikosoa azimio hilo na kulitaja kuwa la kukurupuka na lisilo na busara, na inakanusha madai ya kutengeneza silaza za nyuklia, ikisema mpango wake wa atomiki ni kwa matumizi ya amani na ya kiraia.