Ufaransa yasubiri uteuzi wa serikali mpya
22 Desemba 2024Ufaransa inasubiri uteuzi wa baraza jipya la mawaziri kabla ya sikukuu ya Krismasi, litaloiondowa nchi hiyo katika mgogoro wa kisiasa.
Rais Emmanuel Macron anatarajiwa leo Jumapili kufanya mazungumzo na waziri mkuu Francois Bayrou aliyemteuwa Desemba 13.
Soma zaidi. Kimbunga Chido chauwa watu 13 Malawi na kuwaathiri 45,000
Vyanzo vya habari nchini Ufaransa vinasema kwamba baraza jipya la mawaziri la waziri mkuu Bayrou huenda likatangazwa leo, kwasababu kesho Jumatatu ni siku iliyotengwa kwaajili ya kuomboleza maafa yaliyosababishwa na kimbunga Chido katika kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte.
Kinachopewa kipaumbele na waziri mkuu Bayrou ni kuhakikisha serikali yake mpya itafanikiwa kutopigiwa kura ya imani bungeni na kupitisha bajeti ya mwaka ujao.