MigogoroChina
Ufilipino yaishutumu China kutaka kupoka eneo la bahari
11 Mei 2024Matangazo
Katika taarifa, ofisi ya Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr, imesema kuwa walinzi wa Pwani wametuma meli kufuatilia kile kinachodaiwa kuwa shughuli haramu za China, za kuunda "kisiwa bandia", na kuongeza kuwa meli nyingine mbili hupelekwa kwa zamu katika eneo hilo.
Msemaji wa walinzi wa Pwani ya Ufilipino Commodore Jay Tarriela, ameliambia kongamano moja kuwa kumekuwa na uboreshaji wa kiwango kidogo wa eneo la bahari la Sabina Shoal, na kwamba huenda China ndio iliyohusika katika uboreshaji huo .
Ubalozi wa China mjini Manila haukujibu mara moja ombi la tamko kuhusu madai hayo ya Ufilipino, ambayo huenda yakaongeza tofauti zilizoko baina ya nchi hizo mbili.