1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugaidi katika Pwani ya Kenya

9 Mei 2019

https://p.dw.com/p/3IEM6

Ugaidi ni mfumo wa kulenga mabadiliko ya kisiasa kwa kuwatisha watu kwa njia ya vurugu au mauaji. Matendo ya kigaidi yanatisha kwa sababu watu wanajeruhiwa au kuuawa. Wanaofanya ugaidi kwa kawaida ni vikundi au watu wasio na cheo au nafasi rasmi.
Mara nyingi si rahisi kutofautisha kati ya magaidi, wapinzani wa uhuru au watu wanaoendesha vita vya msituni. Hata majeshi rasmi ya serikali yanaweza kutumia mbinu za kigaidi, lakini kwa kawaida hawahesabiwi kati ya magaidi. Katika kipindi cha Makala Yetu Leo, Shisia Wasilwa anaangazia ugaidi katika Pwani ya Kenya