Uganda yajitenga na msimamo wa Sebutinde katika ICJ
28 Januari 2024Matangazo
Serikali ya Uganda kupitia taarifa yake imesema kwamba msimamo uliochukuliwa na Jaji Sebutinde ni wake binafsi, na hauakisi kwa njia yoyote nafasi ya serikali ya Jamhuri ya Uganda.
Soma pia: ICJ yatambua hatari ya kimbari Ukanda wa Gaza
Aidha iliongeza kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki inaunga mkono msimamo wa vuguvugu la mataifa yasiyofungamana na upande wowote kwenye mzozo huo, uliopitishwa katika mkutano mkuu uliofanyika katika mji mkuu Kampala mwezi huu.
Sebutinde ni moja kati ya majaji wawili kwenye jopo la wanachama 17 waliopiga kura ya kupinga hatua zilizopitishwa na mahakama ya ICJ katika kuiamuru Israeli kuchukua hatua kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki wakati ikipambana na wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.