1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda yapata shinikizo juu ya muswada dhidi ya LGBTQ

22 Machi 2023

Uganda imeendelea kupata shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa na kuitaka isitekeleze sheria kali dhidi ya wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

https://p.dw.com/p/4P5RA
Uganda führt drakonisches Anti-Schwulengesetz ein
Picha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Mkuu wa Haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Volker Turk pia amemtaka Rais Yoweri Museveni kutoiidhinisha sheria hiyo, kwani itawafanya wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda kuandamwa kama wahalifu kwa sababu ya hali zao.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken pia ameitaka Uganda kutoitekeleza sheria hiyo akisema itahujumu haki muhimu za binadamu na itarudisha nyuma mafanikio ambayo yamepatikana kwenye vita dhidi ya virusi vya ukimwi.

Shirika la Amnesty International, limemhimiza Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuukataa muswada huo.

Tigere Chagutah, mkurugenzi wa Amnesty International kanda ya Afrika Mashariki na Kusini amesema sheria hiyo itaanzisha ubaguzi na chuki dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Kulingana na muswada huo yeyote anayeshiriki vitendo vya kishoga anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela.