1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Uganda yasafirisha bangi kwenda Ujerumani

20 Oktoba 2021

Biashara ya bangi inayotumiwa kwa matibabu imeanza kuiletea Uganda fedha za kigeni baada ya kampuni yenye leseni ya kufanya biashara ya bangi kusafirisha shehena ya kwanza ya bangi ya kilo 800.

https://p.dw.com/p/41uWq
Picha ya maktaba inayoonyesha bangi kutoka Colombia ambayo hutumiwa kama dawa dhidi ya baadhi ya maradhi.
Picha ya maktaba inayoonyesha bangi kutoka Colombia ambayo hutumiwa kama dawa dhidi ya baadhi ya maradhi.Picha: RAUL ARBOLEDA/AFP/Getty Images

Kulingana na wataalamu bangi hiyo hutumiwa katika matibabu ya magonjwa mengi sugu ikiwemo saratani.

Awali, kampuni hiyo ilisafirisha shehena  ya kilo mia sita.

Wizara ya afya Uganda imefafanua kuwa inaendelea kupokea maombi kutoka kwa makampuni mbalimbali yakitaka kushiriki biashara hii, lakini inachukua tahadhari kutoa leseni ili bangi hiyo isiishie kutumia kama dawa ya kulevya.

Kulingana na kampuni iliyopanda na kutengeneza aina hiyo ya bangi ya matibabu, wana hadi aina 30 za dawa kwa ajili ya matibabu mbalimbali na ina uwezo wa kusazlisha hadi tani 30 kila mwaka.