Ugiriki yaahidi msaada zaidi kwa visiwa vya Crete na Gavdos
2 Aprili 2024Baada ya ziara katika visiwa viwili vya Crete na Gavdos, waziri wa uhamiaji wa Ugiriki Dimitris Kairidis, alisema watazisaidia jamii za maeneo hayo na kuongeza kwamba kuna raslimali na njia za kutosha kufanikisha hilo.
Idadi ya wahamiaji yaongezeka visiwani Crete na Gavdos
Katika miezi ya hivi karibuni, visiwa vya Crete na Gavdos, vimeshuhudia ongezeko kubwa la wahamiaji lisilo la kawaida zaidi kutoka Misri, Pakistan na Afghanistan.
Soma pia:Wahamiaji 100 waokolewa pwani ya Ugiriki
Takwimu za walinzi wa Pwani ya Ugiriki, zinaonesha kuwa tangu mwezi Januari, zaidi ya wahamiaji1,180 waliwasili kwenye visiwa hivyo viwili, hili likiwa ongezeko kutoka idadi ya wakimbizi 686 waliowasili visiwani humo mwaka mzima wa 2023.
Visiwa vyote viwili vya Gavdos na Crete, havina vituo vya kuwapokea wahamiaji.