1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUholanzi

Uholanzi yatafakari kupeleka waomba hifadhi Uganda

17 Oktoba 2024

Uholanzi inatafakari kuwapeleka Uganda watu wanaotafuta hifadhi ambao maombi yao yamekataliwa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4lu8H
Wahamiaji kutoka Libya
Kulingana na mpango huo, Uganda itawaweka waomba hifadhi hao katika kambi na badala yake ipokee fedha kutoka Uholanzi.Picha: Hamza Turkia/Xinhua/IMAGO

Haya yamesemwa na waziri wa biashara za kigeni na misaada ya maendeleo, wa Uholanzi Reinette Klever.

Klever aliyekuwa akizungumza na kituo cha televisheni cha NOS alipolizuru taifa hilo la Afrika Mashariki, amesema mpango huo unawahusu wahamiaji wa Afrika ambao hawakubaliwi kukaa Uholanzi na ambao hawawezi pia kurudi katika nchi zao za nyumbani.

Waziri huyo amesema kulingana na mpango huo, Uganda itawaweka waomba hifadhi hao katika kambi na badala yake ipokee fedha kutoka Uholanzi.

Serikali ya muungano ya Uholanzi inataka kupitisha sheria kali za kutafuta hifadhi na kupunguza idadi ya wakimbizi nchini humo.