Uingerea yaionya Ulaya kuhusu Brexit
29 Julai 2019Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza Dominic Raab amesema anahitaji makubaliano lakini Umoja wa Ulaya unapaswa kubadili msimamo wake. Amesema katika Umoja wa Ulaya itashikilia msimamo wake Uingereza itapaswa kujianda na kuondoka pasipo makubaliano yoyote. Kimsingo kwa upande wao wanataka makubaliano mazuri.
Boris Johnson na ziara ya kwanza huko Scotland
Katika hatua nyingine waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Boris Johson leo hii anafanya ziara yake ya kwanza ya kikazi, nchini Scotland kama waziri mkuu akiahidi kuimarisha mahusiano baina pande hizo mbili pamoja. Boris Jonhson anafanya ziara wakati akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa viongozi wa Scotland, kutokana na msimamo wake wa kile anachokirejea mara kwa mara kwamba yupo tayari kuiondoa Uingerza katika Umoja wa Ulaya, iwe kwa makubaliano au hata yasiwepo. Katika ziara hii Johnson anatarajiwa kutanagaza kitita cha pauni milioni 3000, kikiwa na lengo la kuchochea uchumi wa Scotland, Wales na Ireland ya Kaskazini.
Waziri wa kwanza wa Scotland Nicola Sturgeon na mwenzake wa kisiwa cha Wales, Mark Drakeford, wote kwa pamoja wamesema litakuwa jambo lisiloeweka kwa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya pasipokuwa na makubaliano yoyote. Lakini nchini Uingereza Jeremy Corbyn ni kiongozi wa chama cha Labour anasema "Bunge linaketi Septemba. Na nafikiri katika kipindi hicho, tutathimini hali ilivyo. Lakini pia juu ya kile atakachokiamua waziri mkuu. Nini ataamua kufanya, kwa sababu kama atajaribu kutoandoa bila makubaliano mwishoni mwa Oktoba, tutaipinga hatua hiyo."
Onyo la wenye viwanda kuhusu Brexit
Katika muendelezo wa vute nikivute ya suala la Brexit kundi kubwa la wafanyabiashara nchini Uingereza limeonya kwamba si upande wa Uingerza wala Umoja wa Ulaya ambao hadi sasa umejiandaa vyema katika hatua ya Uingerza kujiondoa katika umoja wa Ulaya wenye jumla ya mataifa 28.
Shirikisho la wenye viwanda la Uingereza limetoa ripoti yenye mapendekezo 200 kwa pande zote, yenye kuhakikisha mwenendo wa Brexit. Ripoti hiyo imehitimishwa kwa maneno yasemayo "Umoja wa Ulaya unaburuzwa na Uingereza katika jitihada za kudhibiti athari mbaya zaidi za tukio la kujitoa pasipo makubaliano"
Shirikisho hilo limesema serikali ya Uingereza inapaswa kuanzisha upya mikutano ya Brexit na viongozi wa wafanyabiashara na kutenga moda zaidi wa kuridhia sheria zenye kuhusiana na athari za Uingerza kujiondoa bila ya makubaliano katika Umoja wa Ulaya.