1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza: Tutumia mkakati mpya kuboresha uhusiano na Afrika

Hawa Bihoga
3 Novemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy ametangaza "mkakati mpya" na Afrika ambapo nchi hiyo itakuwa msikilizaji "badala ya muelekezaji" akisema mkakati huo utatoa ushirikiano wa heshima baina ya pande mbili.

https://p.dw.com/p/4mXfK
Uingereza | Afrika | Keir Starmer na David Lammy
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akiwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje David Lammy wakiteremka kwenye ndege.Picha: Stefan Rousseau/REUTERS

Lammy amesema hayo muda mfupi alipoanza ziara yake ya kuelekea barani Afrika akizitembelea nchini Nigeria na Afrika Kusini. Amesema, katika ziara hiyo atasikiliza zaidi kutoka kwa washirika wa Uingereza Afrika ili waweze kukuwa kwa pamoja kiuchumi.

Hii ni ziara yake ya kwanza barani Afrika kama Waziri wa Mambo ya Nje na akiwa nchini Nigeria anatarajiwaa kusaini mkataba wa "ushirikiano wa kimkakati" ambao utashughulikia ukuaji, usalama wa taifa na mabadiliko ya tabianchi. 

Soma pia:David Lammy kuhudhuria mazungumzo ya Umoja wa Ulaya

Aidha ofisi yake ilisema akiwa ziarani Afrika Kusini ataridhia kuundwa kwa "Mpango mpya wa Kukuza Uchumi wa Uingereza na Afrika Kusini," mbali na mambo mengine.