UchumiUingereza
Uingereza yajiunga na ukanda wa biashara wa Indo-Pasifiki
15 Desemba 2024Matangazo
Hatua hii ya Uingereza inasifiwa kama mpango mkubwa zaidi wa kibiashara wa taifa hilo, tangu mchakato wa kujiondoa Umoja wa Ulaya - Brexit.
Uingereza sasa inatambulika rasmi kuwa mwanachama wa 12 wa kanda hiyo inayojulikana kama CPTPP, baada ya kutia saini ya kujiunga mwaka uliopita.
Maafisa wanataraji kwamba unachama wa Uingereza utaimarisha uchumi wake kwa hadi pauni bilioni 2.0 kwa mwaka.
Ushirika huo unajumuisha mataifa ya G7, yenye uchumi mkubwa zaidi ulimwenguni, Canada, Japan, pamoja na washirika wa muda mrefu Australia na New Zealand, Brunei, Chile, Malaysia, Mexico, Peru, Singapore na Vietnam.