Ujerumani kupendekeza hatua ya kuwasajili vijana jeshini
12 Juni 2024Matangazo
Haya ni kulingana na shirika la habari la Ujerumani, DPA. Hatua hii ya Pistorius inakuja miaka 13 baada ya Ujerumani kufutilia mbali sharti la vijana kusajiliwa jeshini.
Shirika la habari la DPA linaeleza kwamba pendekezo hilo la Pistorius halitorudisha hatua hiyo ya vijana kusajiliwa kwa mafunzo ya jeshi kwa lazima ila watahitajika kutoa taarifa kuhusiana na iwapo wako tayari kuhudumu jeshini kwa hiari.
Waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani atabainisha yote yaliyoko kwenye mpango wake Jumatano 12.06.2024. Ingawa Ujerumani ilifutilia mbali sheria hiyo ya vijana kulazimishwa kujisajili jeshini, sheria iliyopo bado inatoa uwezekano wa hilo kufanyika endapo kuna vita au mivutano mingine.