1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

Ujerumani kuwasaidia Wakurdi walioachwa bila makaazi

8 Machi 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock amewahakikishia Wakurdi wa Irak msaada mkubwa kwa ajili ya kurejeshwa kwa karibu wakimbizi wa ndani milioni moja.

https://p.dw.com/p/4OPVf
Irak Außenministerin Baerbock und Ministerpräsident Barsani in Erbil
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock amewahakikishia Wakurdi wa Irak msaada mkubwa kwa ajili ya kurejeshwa kwa karibu wakimbizi wa ndani milioni moja kufuatia ushindi wa kijeshi dhidi ya kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu. Akizungumza baada ya kukutana na Masrour Barzani waziri mkuu wa maeneo yanayojitawala ya Kikurdi kaskazini mwa Iraq katika mji mkuu wa mkoa huo Erbil, Baerbock amesema hakuna anayetaka kuishi kwenye kambi maisha yao yote. Barzani alisema serikali ya kikanda inatumai kufanya uchaguzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, baada ya kuahirishwa mwaka jana.

Baerbock amesema makundi ya nje na ndani yanajaribu kuigawa nchi na kulidhoofisha jimbo hilo kwa lengo la kupinga maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Alikuwa anamaanisha mashambulizi yanayoendelea kufanywa kutoka Iran na Uturuki kaskazini mwa Irak pamoja na mizozo ya ndani ya Kikurdi.