Ujerumani yaagiza kufungwa kwa balozi tatu ndogo za Iran
31 Oktoba 2024Sharmahd, mwenye umri wa miaka 69, aliauwa siku ya Jumatatu kutokana na mashtaka ya ugaidi. Haya ni kwa mujibu wa idara ya mahakama ya Iran.
Hatua hiyo inafuatia kesi ya mwaka 2023 ambayo Ujerumani, Marekani na makundi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yaliipuuza na kuiita ya uongo.
Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani tayari ilikuwa imemuita afisa mkuu wa kidiplomasia wa balozi hizo ndogo za Iran kulalamika kuhusu mauaji ya Sharmahd.
Balozi wa Ujerumani Markus Potzel, pia alimlalamikia Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, kabla ya kuitwa Berlin kwa mashauriano.
Uamuzi wa kufungwa kwa balozi hizo ndogo mjini Frankfurt, Hamburg na Munich, kulikotangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock kunaliacha taifa hilo la Kiislamu na ubalozi mmoja tu mjini Berlin.