SiasaBrazil
Ujerumani yaahidi kusaidia ulinzi wa msitu wa Amazon
31 Januari 2023Matangazo
Ujerumani imeahidi kutoa msaada wa Euro milioni 200 kuisaidia Brazil kuulinda msitu wa mvua wa Amazon. Tangazo hilo limetolewa wakati wa ziara ya Kansela Olaf Scholz mjini Brasilia. Scholz ambaye anaizuru Brazil baada ya kuzitembelea Chile na Argentina, amesema amefurahishwa na kurejea kwa Brazil katika jukwaa la dunia. Msaada huo unajumuisha mfuko mpya wa euro milioni 31 kwa ajili ya majimbo ya Brazil kusaidia ulinzi wa msitu huo, na euro milioni 93 zitaelekezwa kwenye miradi ya upandaji tena miti. Kansela wa Ujerumani amesema Berlin inataka maendeleo ya haraka katika makubaliano ya biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya na jumuiya ya Mercosur.